Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Refa aliewapa bao Liverpool apewa Arsenal

Paul Tierney Vv Refa aliewapa bao Liverpool apewa Arsenal

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwamuzi, Paul Tierney ameondoshwa kwenye orodha ya marefa watakaochezesha mechi zijazo za Ligi Kuu England baada ya kuwasaidia Liverpool kupata bao la utata kwenye dakika za majeruhi dhidi ya Nottingham Forest wikiendi iliyopita.

Mwamuzi huyo amekosolewa sana baada ya kuwamilikisha mpira Liverpool na kuwaruhusu kufanya mashambulizi yaliyozaa bao la dakika za majeruhi lililofungwa na straika Darwin Nunez.

Beki wa Liverpool, Ibrahima Konate alianguka baada ya kuumia kichwa wakati Forest wakipiga kona baada ya kugongana na kipa wake, Caoimhin Kelleher.

Licha ya kwamba wakati filimbi ya kusimamisha mpira inapulizwa, umiliki wa mpira kuwa kwa Forest kupitia staa wao Callum Hudson-Odoi, lakini Tierney alipoanzisha tena mechi, alimpa mpira kipa wa Liverpool, Kelleher, ambapo lilianzishwa shambulizi la haraka na Liverpool kwenda kufunga bao pekee.

Tierney sasa ameadhibiwa kwa kuotolewa kwenye orodha ya waamuzi watakaochezesha mechi wikiendi hii.

Hata hivyo, bado amepewa majukumu ya kusimamia kwenye VAR wakati wa mchezo wa Arsenal na Brentford utakaopigwa Jumamosi uwanjani Emirates.

Jambo hilo limewashtua mashabiki wa Arsenal na kusema: "Kwanini wametupa sisi Paul tierney?"

Mwingine aliongeza: "Hapana aisee. Siku zote wanataka tu kutuharibia."

Shabiki wa tatu aliandika: "Bila shaka huko kwenye VAR atataka kutuharibia ili kuwabeba Liverpool."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live