Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Refa afungiwa baada ya kujichagua kuchezesha mechi Sauzi

Redcard1280 Refa afungiwa baada ya kujichagua kuchezesha mechi Sauzi

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Afrika Kusini zinaeleza kuwa, mwamuzi Bethuel Makgato amefungiwa na Shirikisho la soka nchini humo SAFA baada ya kujiamulia kuchezesha mchezo wa Ligi ya ABC Motsepe bila kamati ya waamuzi kujua.

Makgato alichukua uamuzi huo baada ya maafisa waliokuwa wameteuliwa kusimamia mchezo huo kuchelewa kufika kutokana na tatizo la usafiri na hakuwapa taarifa kamati ya waamuzi.

Hii si mara ya kwanza kwa mwamuzi huyo kufungiwa kwani mwaka 2022 alifungiwa pia baada ya kutoa nyekundu mbili kwa timu moja kwenye mchezo wa kuepuka kushuka daraja kwenye Ligi hiyo hiyo ya ABC Motsepe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live