Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Refa Bora atangaza kustaafu

Untitled Gassama Bakary Papa Gassama

Sat, 23 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwamuzi bora wa muda wote Barani Afrika Bakary Papa Gassama kutoka nchini Gambia leo rasmi ametangaza kustaafu kazi hiyo akiwa na umri wa miaka 44.

Gassama amewahi kuchezesha michuano ya Olympic mwaka 2012, ambapo alikuwa mwamuzi wa mezani katika mchezo wa Mexico dhidi ya Brazil.

Gassama alianza kuwa mwamuzi rasmi mwaka 2007 akichezesha michezo mbalimbali ya Ligi kuu nchini Gambia kwa uwezo mkubwa.

Hadi kufikia kustaafu kwake amechezesha michezo na mashindano yote makubwa yaliyofanyika Barani Afrika ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika, kombe la shirikisho na AFCON.

Unamkumbuka kwa mechi gani aliyokukosha zaidi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live