Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Reece James ndio basi tena England

Reece James Missout Beki wa Chelsea, Reece James

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kulia wa wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza Reece James ametangaza mwenyewe kua hataweza kushiriki michuano ya kombe la dunia yatakayofanyika nchini Qatar mwezi huu.

Beki huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye anauguza majeraha yake ya goti kupitia mtandao wake wa Twitter ameonesha kusikitishwa kutokuwepo nchini Qatar kulipambania taifa lake, N hiyo ni kutokana na kuona kila dalili ya kutokupona goti lake zikiwa zimebakia siku 11 kuanza kwa michuano hiyo.

Reece James anasema alikua anajua ingekua ngumu kurudi kua fiti na kuiwakilisha Uingereza kwenye michuano hiyo lakini bado aliamini ingewezakana kwasababu alikua anapambana kuhakikisha anakuepo kwenye michuano hiyo ili kulipambania taifa lake.

Lakini pamoja na kutokuepo kwake Reece James amewatakia kila la heri wenzake kuelekea kwenye michuano hiyo itayoanza kutifua vumbi Qatar Novemba 20.

Pamoja na hivo kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza bado hakijatangazwa kuelekea kombe la dunia, Lakini kuna kila dalili ya kutangazwa kesho kama leo itapita kwani kesho ndo mwisho wa kutangaza vikosi vya timu za taifa kutokana na maelekezo ya Fifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live