Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Reece James amtembelea Shabiki aliezimia

Reece James Hospital Reece James amtembelea Shabiki aliezimia

Sat, 18 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki wa Chelsea, Reece James ametuma ujumbe wenye hisia kupitia akaunti ya Instagram baada ya kumtembelea hospitali shabiki aliyepatwa na mshtuko wa moyo.

Tukio la shabiki huyo aliyezimia kwa dakika 20 kutokana na mshtuko wa moyo lilitokea wakati wa mechi ya Ligi Kuu England kati ya Chelsea na Manchester City kabla ya mapumziko ya kimaitaifa timu hizo zikitoka sare ya mabao 4-4.

Hata hivyo, wakati mechi inaendelea shabiki huyo wa Chelsea alipatwa na mshtuko akiwa jukwaani uwanjani Stamford Bridge na kuzua taharuki. Shabiki huyo alidondoka na kuzimia kwa dakika 20 wengi wakiamini kwamba huenda amefariki, lakini baada ya kufanyiwa matibabu alizinduka. Kwa sasa anaendelea kupata nafuu hospitalini na wiki hii alitembelewa na nahodha huyo wa Chelsea ili kumsaidia na kumpa moyo kufuatia mshtuko huo.

Beki huyo aliandika ujumbe wa maneno kupitia akaunti yake yenye wafuasi milio 3.1 akisema:

“Nilitembelea hospitali jioni ya leo kumona shabiki wa Chelsea ambaye alipata mshtuko wa moyo kwenye mchezo wetu dhidi ya Man City. ‘Alifariki’ kwa dakika 20 na madaktari walifanikiwa kuokoa maisha yake. Alionekana mwenye nguvu . Nina furaha sana kwamba amepona.”

James aliendelea kusema: “Maisha ni ya thamani sana na hayatabiriki. Kila kitu kinaweza kutokea wakati wowote. Kwa hiyo furahia maisha hata kama wakati mwingine mambo yanakuwa magumu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live