Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Reece: Enzo anakuja kuharibu

Enzo X Reece Reece: Enzo anakuja kuharibu

Sun, 28 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa Chelsea, Reece James amesema kurejea kwa kiungo Enzo Fernandez katika kikosi chao kesho inaweza kusababisha matatizo kutokana na wachezaji wengi kuwa bado wamekasirishwa na video yake iliyosambaa akiimba nyimbo ya kibaguzi.

Enzo ataungana na wachezaji wenzake katika kikosi hicho cha Chelsea kilichopo Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Reece ambaye pia ni nahodha wa Chelsea aliyasema hayo alipokuwa anafanya mahojiano na waandishi wa habari katika kambi yao huko Marekani.

“Bila shaka hakutokuwa na usawa. Siku zote watu hawawezi kuwa sawa kunapokuwa na tatizo, lakini najua kuna siku mambo yanaweza kuwa sawa na kila mtu atakuwa na furaha na mwenzake na tutasonga mbele,” alisema Reece alipoulizwa juu ya suala hilo.

“Nilizungumza naye kidogo (Enzo), lakini ilikuwa ngumu kwa sababu tulikuwa katika maeneo tofauti ambayo yalikuwa yakipishana kimasaa, nilizungumza naye kuhusu vitu vingi ikiwa pamoja na maoni yake juu ya kile kilichotokea, alijaribu kunielezea hali yake, kwa kweli ni jambo gumu sana na kwenye mpira wa miguu hakuna nafasi ya ubaguzi wa rangi.”

Kwa sasa Fernandez bado yuko chini ya uchunguzi wa mamlaka za soka kutokana na wimbo wake aliokuwa akiimba kuhusu wachezaji wa Ufaransa muda mchache baada ya kushinda taji la Copa America akiwa na timu ya taifa ya Argentina.

Wakati Reece anaona kama itakuwa ni tatizo, kocha wa timu hiyo Enzo Maresca yeye haamini kama kutakuwa na tatizo lolote kwa urejeo wa fundi huyo wa boli.

“Nafikiri kuna urahisi kwa sababu mchezaji mwenyewe ameshaomba msamaha na timu nayo imefanya hivyo, mwisho wa yote wachezaji wote ni binaadamu, sioni kama kutakuwa na shida yoyote baina yao pale atakaporejea, sidhani kama kuna cha kuongeza, wachezaji wenzake pia wanafahamu kwamba yeye sio mtu mbaya, kilichotokea ni hali ya kibinadamu.”

Enzo anatarajiwa kujiunga na wenzake kesho Jumatatu.

Chanzo: Mwanaspoti