Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Redknapp : Lukaku awewarudisha Chelsea kwenye mbio za Ubingwa

Romelu Lukaku Chelsea  768x432 Lukaku akiifungia Chelsea goli

Tue, 28 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa Soka, Jamie Redknapp amesema mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku amewarejesha kwenye mbio za ubingwa baada ya kiwango alichoonyesha katika mchezo dhidi ya Aston Villa.

Lukaku hajacheza katika mechi kumi na moja (11) kwenye ligi kuu ya EPL kutokana na majeraha wakati goli lake la mwisho kufunga likiwa ni mwezi septemba.

“Uwezo wa Lukaku akiwa mwenyewe kwenye ushambuliaji umewafanya warejee kwenye mbio za ubingwa.” alisema Redknapp

“Walikuwa wanahitaji kitu cha kuwapa motisha na hicho ndicho alicholeta kwenye timu. Kipindi cha kwanza hawakuweza kwenda mahala popote kwa haraka, meneja alikuna kichwa kujua nini cha kufanya.

“Kitu pekee ilikuwa nikumuweka uwanjani, kwasababu walipata shida Christian Pulisic kama namba tisa ya uongo.

“Lakini kama Chelsea watatwaa ubingwa mbele ya City na Liverpool, Lukaku anachukua nafasi kubwa.” aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live