Kwenye mchezo wa juzi wa La Liga dhidi ya Villareal, kocha wa Real Madrid Carlo Acelotti alianzisha kikosi chenye wachezaji wa kigeni tupu.
Hii ilikuwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 120 ya klabu hiyo kuanza mchezo bila kuwa na mchezaji hata mmoja raia wa Hispania,
Hii inakuja siku moja baada ya kifo cha Gianluca Vialli, aliyekuwa kocha wa Chelsea mwishoni mwa miaka ya 1990 hadi mwaka 2000.
Disemba 26, 1999, Vialli aliandika historia kwenye soka la England kwa kuanzisha kikosi cha wageni watupu.
Ilikuwa dhidi ya Southampton ambapo Vialli aliwashangaza wengi kwa kutompanga hata mchezaji mmoja raia wa England.
Kwa kufanya hivyo, Vialli alivunja utamaduni uliodumu kwa miaka 111, miezi mitatu na siku 17 katika mechi 150,000.
Ancelotti na Vialli walikuwa marafiki na walicheza wote timu ya taifa ya Italia kuanzia 1985 pale Vialli alipoitwa kwa mara ya kwanza, hadi 1991 pale Ancelotti alipostaafu.