Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Real Madrid washusha dozi nzito kwa Liverpool Uwanja wa Anfield

Karima Benzema Goal Karim Benzema alifunga mabao mawili mchezo wa jana

Wed, 22 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majogoo wa Jiji, Timu ya Liverpool imekubali kichapo cha 5-2 dhidi ya Mabingwa wa Dunia, Real Madrid katika dimba la Anfield.

Mchezo huo wa hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya iliwashuhudia Liverpool wakianza mchezo kwa kasi na kupata mabao ya haraka kupitia kwa Darwin Nunez na Mohammed Salah.

Alikuwa ni Vinicious Junior aliepachika mabao mawili na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko matokeo yakiwa mabao 2-2.

Kipindi cha pili Real Madrid walirudi na makakati madhubuti na kufanikiwa kupachika mabao matatu yaliyofungwa na Karim Benzema aliefunga mawili na E. Militao.

Mpaka dakika 90 zinakamilika Liverpool walikubali unyonge Uwanja wao wa nyumbani ambao unaogopwa na vilabu vingi Barani Ulaya.

Majogoo wa Jiji wana kazi kubwa kwenye mchezo wa marudiano ili kufuzu hatua inayofuata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live