Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Real Madrid waichapa Valencia, Vinicius akionesha maajabu

Madrid Vs Valencia Real Madrid waichapa Valencia, Vinicius akionesha maajabu

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Real Madrid imeichapa Valencia 2 – 0 na kupunguza pengo la pointi na kinara FC Barcelona ambao walishinda Jumanne kwa Real Betis ukiwa ni mwendelezo wa Ligi Kuu ya La Liga.

Ushindi wa Madrid umechagizwa na ubora wa winga wa kimataifa wa Brazil Vinicius Jr ambaye alifunga bao kwenye mchezo wake wa 200 ndani ya Los Blancos bao la kwanza likawekwa nyavuni na Marco Asensio.

Kwa sasa tofauti ya alama tano inatenganisha kati ya Barca na Real.

Valencia walilazimika kumaliza pungufu kufuatia Gabriel Paulista kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye dakika ya 72 baada ya mchezo mbaya kwa Vinicius.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live