Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Real Madrid sasa yamvizia Jesus

G Jesus.jpeg Gabriel Jesus

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kwa mujibu wa ripoti Real Madrid inajiandaa kutuma ofa kwa ajili ya straika Gabriel Jesus anayekipiga Arsenal katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi msimu ujao.

Jesus alihusishwa na Los Blancos kabla ya kujiunga na Arsenal, lakini uhamisho wake ukakwama kutokana na ishu za uhamiaji na pasipoti ya kusafiria.

Hata hivyo, inaleezwa kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti bado anakumbali mchezaji huyo na anaamini atampata siku za usoni baada ya uhamisho wake kukwama msimu huu.

Kwa mujibu wa ripoti, Jesus ni mchezaji wa tano katika orodha ya mastraika anaowataka kocha huyo ndani ya kikosi chake atakayesadiana na Karim Benzima ambaye umri umeanza kumtupa mkono.

Jesus amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Arsenal tangu mwanzoni mwa msimu, lakini sasa kiwango chake kimeanza kushuka kwani hajafunga mabao katika mechi sita mfululizo. Nyota huyo wa zamani wa Manchester City amefunga mabao matano katika mechi 11 alizocheza msimu huu.

Kutokana na ukame wa mabao unaomkabili kwa sasa kocha Mikel Arteta amemtaka mchezaji huyo kupambana kuepukana na hali hiyo.

“Nataka mabao kutoka kwake, huo ndio ukweli, kushinda mechi na kuweka uwiano mkubwa wa pointi dhidi ya wapinzani wetu. Huu ukame wa mabao unatakiwa ukome kwani timu inakuwa haipo katika nafasi nzuri ya kushinda mechi,” alisema Arteta. Jesus hacheka na nyavu walipoibamiza Nottengham Forest mabao 5-0 wikiendi iliyopita.

Chanzo: Mwanaspoti