Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Real Madrid kumsajili jumla Kepa Arrizabalaga

Kepa To Real Kepa Arrizabalaga

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: Dar24

Klabu ya Real Madrid ipo tayari kumsajili jumla Mlinda Lango Kepa Arrizabalaga kutoka Chelsea, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi lakini haipo tayari kulipa zaidi ya Pauni 17.5 milioni.

Mlinda lango huyo raia wa Hispania miaka mitano iliyopita alivunja rekodi ya kuwa kipa ghali zaidi duniani baada ya kusajiliwa akitokea Athletic Bilbao kwa Pauni 71.5 milioni kwenda Chelsea.

Real Madrid imefikia uamuzi wa kumsajili Kepa kutokana na kiwango bora alichoonyesha baada ya kujiunga nayo kwa mkopo katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Tangu msimu huu uanze Real Madrid imepoteza mechi moja ya La Liga wakati Kepa akiwa golini.

Kepa alisajiliwa kwa ajili ya kuziba kwa muda pengo la Thibaut Courtois ambaye atakuwa nje kwa msimu mzima kutokana na majeraha ya goti yanayomsumbua.

lli kufanikisha dili lake, Kepa anadaiwa kukubali hadi kupunguziwa mshahara wa Pauni 175,000 kwa juma anaoupokea ili kuiwezesha Madrid kumchukua. Mkataba wake wa sasa na Chelsea unatarajiwa kumalizika 2025.

Chanzo: Dar24