Mkurugenzi wa michezo wa zamani wa Real Madrid, Pedja Mijatovic amekiri timu hiyo itapata tabu sana bila ya uwepo wa Karim Benzema kufuatia kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Atletico Madrid.
Bosi huyo anadhani kwamba Madrid itaendelea kuteseka zaidi kwani Benzema alikuwa na mchango mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji.
“Hakuna mchezaji mwingine anayekaribia uwezo wa Benzema, unaposhindwa kuwa na takwimu kama zake, hapo utakuwa na tatizo. Kwenye mechi muhimu kama Madrid dabi tumeona tulivyopata tabu. Ndio hiki ni kipindi cha mpito.
Kwenye dirisha la usajili huwezi kushindwa kusajili wachezaji wakubwa, lakini nadhani Madrid inaweza kufanya jambo. Tuvumilie tu msimu huu, sioni tukifanya mambo makubwa kama ilivyokuwa miaka mingine iliyopita,” alisema Mijatovic.