Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Real Madrid, Barcelona kupigana vikumbo London

Gabriel Jesus Injury Real Madrid, Barcelona kupigana vikumbo London

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Klabu za Hispania Real Madrid na Barcelona zinadaiwa kuwa kwenye mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Gabriel Jesus, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kuvutiwa na kiwango bora alichokionyesha tangu asajiliwe na Washika Mitutu hao akitokea Manchester City.

Jesus mwenye umri wa miaka 26, msimu huu amefunga mabao manne kwenye mechi saba za michuano yote, anawindwa na timu hizo mbili kwa sababu umri wake bado unamruhusu na kiwango bora alichonacho licha ya majeraha ya mara kwa mara yanayomuandama.

Timu nyingi zimeonyesha kushawishika na kiwango cha Jesus kwenye Ligi ya Mabingwa kwa msimu huu ambapo amefunga mabao matatu.

Namna pekee ya Jesus kutua Madrid ama Barcelona ni uhitaji wake mwenyewe wa kufanya hivyo lakin ikiwa hatoshawishi kuuzwa kuna uwezekano mkubwa Arsenal ikakataa ofa zitakazowasilishwa mezani kwao.

Chanzo: Dar24