Awali mchezo wa mzunguko wa kwanza timu zote zitoka sare ya bila kwa bila. Huu ukiwa ni mfululizo wa miaka nenda rudi ikishindwa kutinga makundi.
Kwa upande mwingine Rayon Sports mwakilishi wa Rwanda katika mashindano ya Shirikisho pia imeshindwa kusonga hatua ya makundi ya CAF Confederation baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 4-2 na Al-Hilal katika uwanja wa Pele.
Kocha wa timu ya Rayon Sports alikuwa na haya ya kusema baada ya mechi hiyo; "Nasikitika sana kwasababu nilikuja hapa kwa ajili ya kufuzu kwenye makundi ili kurejesha ndoto za mashabiki, wapenzi na timu.
"Nashukuru sana kwa mashabiki amabao wamejitokeza kwa wingi, Rayon ni timu ni nzuri, tumecheza vizuri lakini katika soka bahati pia ni muhimu sana, leo hatukuwa na bahati sasa hatukufuzu ndivo ilivo Bwana."
Mechi ya mzunguko wa kwanza mjini Cairo Arab contractors ilifunga mabao 2-1 mchezo wa marudio Kigali timu hizo zikatoka sare tasa. Rayon ikaaga mashindano ya Kombe la Afrika.
Mwalimu Muhamed Ouda kutoka Misri anayekinoa kikosi cha AL Hilali ya Libya akijigamba baada ya kuwanyuka Rayon kwa njia ya matuta, amesema si mara ya kwanza kuibandua Rayon mashindanoni.
"Mwaka 1996 nilikuwa nikiichezea timu ya Arab contractors tuliwafunga Rayon mabao 2-1 mjini Cairo halafu mchezo wa marudiano katika uwa wa Kigali tukatoka tasa".