Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ratiba ya mechi za Robo Fainali Kombe la Dunia 2022 hii hapa

Morocco 1 Erf Ratiba ya mechi za Robo Fainali Kombe la Dunia 2022 hii hapa

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashindano ya Kombe la Dunia sasa yameingia raundi ya robo fainali baada ya mechi ya mwisho ya hatua ya mwondoano kuchezwa Jumanne usiku.

Siku ya mwisho ya hatua ya mwondoano ilishuhudia Morocco ikifuzu kwa robo fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia. 

Taifa hilo la kaskazini mwa Afrika iliwabwaga mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka wa  2010,  Uhispania katika hatua ya mikwaju ya penalti baada ya mechi kuisha 0-0 baada ya muda wa ziada.

Abdelhamid Sabiri, Hakim Ziyech na Achraf Hakimi walifunga penalti tatu za Morocco huku Uhispania wakishindwa kufunga penalti yoyote kati ya tatu ambazo walipiga. Mlinda lango Yassine Bounou aliibuka bingwa wa mchuano huo.

Morocco sasa itachuana na Ureno katika robo fainali mnamo Jumamosi, Desemba 10. Hii ni baada ya Ureno kupata ushindi mkubwa wa 6-1 dhidi ya washindani wao katika raundi ya mwondoano, Uswizi. Goncalo Ramos (3), Pepe, Raphael Guerreiro na Rafael Leao ndio waliofanikisha ushindi wa Ureno huku beki Manuel Akanji akifungia Uswizi bao la pekee la kufuta machozi.

Timu zingine ambazo zilikuwa zimefuzu awali ni Brazil na Croatia ambazo zitamenyana mnamo Desemba 9, Uholanzi na Argentina ambazo zitachuana siku hiyo hiyo pamoja Uingereza na Ufaransa ambao watamenyana Desemba 10.

Tazama ratiba ya michuano ya robo fainali hapa:-

Chanzo: www.tanzaniaweb.live