Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ratiba kamili Simba, Yanga CAF iko hivi, mashabiki wachekelea

Kikosi Cha Simba SC 1 1140x640 Simba inashiriki Ligi ya Mabingwa

Tue, 13 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya droo ya makundi Klabu bingwa na Kombe la Shirikisho barani Afrika kuchezeshwa jana Desemba 12 mashabiki timu za Yanga na Simba kanda ya Kaskazini wameonyesha matumaini makubwa kwa timu zao kufanya vizuri.

Yanga imepangwa kundi D ya Kombe la Shirikisho ikiwa na timu za TP Mazembe kutoka DRC Congo, US Monastir ya Tunisia na Real Bamako ya nchini Mali ambapo wataanza kuchanga karata zao dhidi ya Us Monastir nchini Tunisia Februari 12 mwaka 2023 kisha kuialika TP Mazembe Februari 19 uwanja wa Taifa Dar.

Simba wenyewe wanashiriki Ligi ya Mabingwa ambapo wamepangwa kundi C na timu za Raja Casablanca kutoka Morocco, Horoya ya Guinea pamoja na majirani zao Vipers SC kutoka nchini Uganda.

Mnyama nae ataanzia ugenini kati ya Februari 10-11 nchini Guinea kumenyana na Horoya kisha kurejea nyumbani kukipiga na Raja Casablanca kutoka Morocco, mchezo ambao utapigwa kati ya Februari 17-18 mwaka 2023 uwanja wa Taifa Dar.

Maulid Rashid ni mwenyekiti wa Yanga tawi la Stendi Kuu ya mabasi Arusha baada ya kushuudia uchezeshwaji wa droo amesema kutokana na timu ambazo wamepangwa nazo haoni wa kuwazuia kwani wana timu nzuri kwa sasa kuwashinda wote.

Amesema kwa sasa Yanga jinsi ilivyo hata kama wangepangwa na timu ya namna gani bado wangetoboa na kufika mbali Kimataifa kwani wachezaji wao wana uzoefu mkubwa na mashindano hayo lakini pia ubora walionao inawabeba.

“Wale Mazembe kwa sasa wako unga siyo wa kuja kutuzuia mimi naona kabisa Yanga msimu huu tunafika hadi nusu fainali na hata fainali kutokana na kikosi chetu kilivyo yani siyo ya mashaka mashaka hata kidogo,” amesema Maulid.

Kwa upande wake mjumbe wa tawi la Simba Himo darajani mjini Moshi, Ponera Peter anasema hana wasiwasi na kikosi chake lakini pia amefurahi kuona wako katika kundi ambalo liwawafanya kutinga hatua ya robo fainali kwa mara nyingine tena.

Amesema hawana mashaka na wachezaji wao lakini pia anajua katika dirisha dogo la usajili kuna nyota kadhaa wataongezwa ili kuja kuongeza nguvu na kuwafanya Simba kutimiza malengo yao ya kufika nusu fainali ambayo wameshindwa kufika baada ya kuingia robo mara mbili.

“Alama zetu sita wanazo hao Vipers alafu hao wengine hata tukichukua tatu tatu siyo mbaya bado itatufanya tuingie robo fainali kwahiyo niseme tu sina wasiwasi na kikosi changu kwanza nimeruhai mno baada ya kuona kundi letu,” amesema Ponera.

Sabrina Salamba ni shabiki wa Yanga anasema kikubwa sasa kwa kamati ya usajili wa timu yao itumie dirisha ndogo vyema ili kuweza kuwapata watu sahii ambao wataongeza nguvu na kuifanya timu yao iweze kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live