Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ratiba Michezo ya Ngao ya Jamii 2024 hadharani

Ratiba Ngao Ya Jamii Ratiba Michezo ya Ngao ya Jamii 2024 hadharani

Mon, 10 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza tarehe rasmi za michezo ya michuano ya Ngao ya Jamii kwa msimu wa 2024-25 ambapo michezo hiyo itachezwa kati ya Agosti 8 hadi Agosti 11, 2024.

Timu 4 ambazo zitashiriki michuano hiyo msimu huu ni Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Yanga SC, Bingwa mtetezi wa Ngao ya Jamii, Simba Sc, Azam FC na Coastal Union.

Aidha taarifa ya TFF haijabainisha ni wapi michezo hiyo itapigwa kwa msimu huu. Msimu uliopita michezo ya Ngao ya Jamii ilichezwa katika dimba la Mkwakwani Jijini Tanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live