Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ratiba Kombe la Mapinduzi hadharani

Mapinduzi Cup Ratiba ya Michuano ya Mapinduzi Cup

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Kandanda Visiwani Zanzibar, limetoa droo ya Kombe la Mapinduzi ambalo kinakusudia kuanza kuchezwa kuanzia Januari Mosi, 2023.

Kwenye droo ambayo imetangazwa Leo kwa vyombo vya habari, bingwa mtetezi wa michuano hiyo maalumu kwa ajili ya kuadhimisha mapinduzi ya Zanzibar klabu ya Simba imepangwa Kundi C pamoja na vigogo wengine kama Mlandege na KVZ.

Kwa upande wao, mabingwa wa Bara, Yanga SC wao wapo Kundi B pamoja na Singida Big Stars na wenyeji, KMKM ambao pia ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar.

Kundi A linaundwa na Azam FC ya Dar es Salaam, wenyeji, Malindi SC na Jamhuri FC ya Pemba.

Wakati Kundi D kuna Namungo ya Lindi, Aigle Noir ya Burundi na Chipukizi ya Pemba.

Nusu Fainali ya kwanza ni mshindi wa Kundi A dhidi ya mshindi Kundi B na ya pili ni mshindi wa Kundi C dhidi ya mshindi wa Kundi D.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live