Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi: Yanga yampa "Thank You" Yanick Bangala

Bangala 91504 Yanick Bangala

Sat, 29 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa ya Yanga kuhusu Yanick Bangala

Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutarifu Umma kuwa tumefikia makubaliano na Klabu ya Azam FC ya kumnunua mchezaji wetu Yanick Litombo Bangala.

Mchezaji Yanick Bangala ameuzwa kwenda Azam FC kwa dau ambalo halitawekwa wazi kutokana na makubaliano ya pande zote mbili.

Bangala alijiunga na Yanga Agosti. 2021 na amekuwa sehemu ya kikosi chetu kilichobeba mataji sita ya mashindano ya ndani pamoja na kuisaidia timu yetu kucheza mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho la CAF msimu uliopita.

Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kumtakia kila la kheri Bangala kwenye timu yake mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live