Uongonzi wa Yanga umefikia makubaliano na Feisal Salamu rasmi kwa kuachana kwa amani baada ya kumaliza mazungumzo yao juzi.
Taarifa zinaeleza, Yanga wamekubali kumuuza Feisal salumu kwenda kwa Klabu ya Azam Fc kwa dau la Tshs 270.4M kiasi ambacho Yanga sc walikiomba Kutoka kwa Azam Fc kununua mkataba wake Kwenye mazungumzo yao hapo jana.
Awali, Azam Fc walifikia dau la 160M lakini Yanga waliligomea dau hilo na kuwalazimu klabu ya Azam Fc kurudi tena na ofa yao ya pili.
Inaelezwa, Yanga itapokea kiasi cha 150M mwishoni mwa mwezi huu Kama ada ya awali ya usajili kutoka kwa Azam FM na baadae Azam Fc watamalizia kiasi kilichobaki cha 120.4M katikati ya mwezi wa 7 mwaka huu.
Kwenye dili hili hakuna makubaliano yoyote Kati ya Yanga na Azam Fc ambalo litamuhusisha Kiungo Akaminko kama sehemu ya dili hili kama Yanga walivyotaka kumjumuisha kiungo Akaminko.
Licha ya kwamba Yanga kutoanika kiasi cha fedha walichomuuza, kupitia ukurasa wao rasmi wa Instagram, leo Juni 8, 2023, wameposti taarifa kwa umma ya kuonesha wamepokea ofa ya Azam na kukubali kumuuza.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Feisal ataungana na timu yake mpya (Azam) mara baada ya kumalizana mambo binafsi na Azam na dirisha la usajili kufunguliwa.