Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi Simba kukutana na 1° de Agosto ya Angola

Desportivo De Agosto Rasmi Simba kukutana na 1° de Agosto ya Angola

Sun, 18 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rasmi Klabu ya soka ya Simba, itakutana katika hatua inayofuata kwenye mashindano ya club bingwa Afrika watakutana na Desportivo 1° de Agosto ya nchini Angola.

FT: Agosto 1-1 Red Arrows AGG 2-1.

Itakumbukwa kuwa De Agosto Walipigwa na Namungo FC, wanarudi mbele ya SIMBA SC

Ni nani hawa "DESPORTVO 1st De Agosto"?

Jina la Utani ni 'Os aglorioso' yaani Watukufu, au 'Os Rubro e Negros' yaani Wekundu na Weusi.

Miamba ya soka kutoka Angola, Klabu ya Jeshi la Angola yenye misuli mikubwa ndani ya Angola na Africa kwa Ujumla.

De Agosto, inashika nafasi ya 2 Kwa mafanikio nyuma ya Petros Atletico De Luanda ambao wanamilikiwa na Kampuni ya Mafuta ya Sonangol.

De Agosto Miaka mingi Imekua ikishiriki michuano ya CAF lakini Kwa Miaka ya karibuni ilifika hatua ya nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa kabla ya kutolewa na Esperance (Mabingwa) Kwa Aggregates ya 4-3.

Agosto waliyumba Miaka ya 2019, 20 na 21 kutokana na janga la Corona ambalo liliathiri sana soka la Angola Kwa ukubwa wake

Msimu huu wamerejea tena kusaka ubora wao baada ya Misimu mitatu kupita bila kufanya vizuri CAF, Na Misimu miwili nyuma walitolewa na Namungo FC.

Mchezo wa kwanza Utacheza ANGOLA Oktoba 7-9 kisha Marudiano yatafanyika Dar Es Salaam OKTOBA 14-16.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live