Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi Ratcliffe akabidhiwa Man United

Sir Jim Ratcliffe Ew Rasmi Ratcliffe akabidhiwa Man United

Mon, 25 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hii inaweza ikawa taarifa njema kwa mashabiki wa Manchester United, baada ya kusubiri kwa muda mrefu mchakato wa uuzwaji wa klabu yao hiyo.

Rasmi, sasa taarifa zinasema mwekezaji mpya wa klabu hiyo, bilionea Sir Jim Ratcliffe amethibitishwa kuchukua umiliki wa asilimia 25 za hisa za klabu hiyo, kwa Pauni 1.25 bilioni na dili hilo litaifanya kampuni ya INEOS kuhusika na mambo ya uendeshaji wa klabu ikiwamo kuwa na kauli kwenye masuala ya biashara yanayoongozwa na Familia ya Glazers.

Hata hivyo, tofauti na inavyodhaniwa na mashabiki wa timu hiyo hasa kipindi hiki cha kuelekea dirisha la usajili la Januari, Man United haitarajii kuwa bize na masuala ya usajili. Ratcliffe na timu yake ya INEOS watadhibiti masuala yote ya wachezaji pamoja na kufanya usajili katika madirisha mabalimbali.

Hata hivyo, bilionea huyo atatangazwa baada ya kupitishwa na Ligi Kuu England mchakato ambao unaweza kuchukua kati ya wiki sita hadi nane.

Ahadi ya Pauni 245 milioni kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Old Trafford na uwanja wa mazoezi wa Carrington zitatekelezwa mara tu bilionea huyo atakapoanza majukumu yake.

Pia imeelezwa bilionea huyo anataka kupitisha panga la wachezaji na uongozi kwenye bodi kama sehemu ya mabadiliko mapya.

Mail Sport iliripoti wiki hii Ratcliffe, 71, atapunguza wafanyakazi katika idara mbalimbali baada ya kukabidhiwa timu. Tathmini ya umakini imetoa taarifa Man United ina wafanyakazi wengi katika idara tofauti na itafanyiwa marekebisho Ratcliffe atakapoanza majukumu yake.

Man United ina wafanyakazi wengi zaidi kuliko klabu yoyote Ligi Kuu England, ikiwa na zaidi ya wafanyakazi 1100 kwenye orodha ya malipo huko Old Trafford.

Tajiri huyo alimshinda mwekezaji kutoka Qatar, Jassim Bin Hamad Al Thani, ambaye alitaka kununua hisa zote, hata hivyo Glazers ikampotezea ofa yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live