Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi:Paulo Dyabala atua As Roma

Dyabala Paulo Gh.jpeg Dyabala atambulishwa As Roma

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fowadi wa kimataifa wa Argentina Paulo Dybala amejiunga na AS Roma inayoshiriki Ligi Kuu nchini Italia Seria A kama mchezaji huru ambapo amemwaga wino wa miaka mitatu.

Dybala nyota mwenye umri wa miaka 28 anajiunga na timu hiyo inayonolewa na kocha Jose Mourinho baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu na Juventus.

Anaondoka Juve akiwa amecheza jumla ya mechi 293 na mabao 115 ambapo amecheza mechi tangia mwaka 2015 akitokea Palermo.

Dybala anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na kocha Mourinho kwenye majira ya kiangazi, nyota wengine ni Nemanja Matic kutokea Manchester United, kipa wa Antwerp Mile Svilar, na mlinzi wa Lille Zeki Celik.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live