Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi! Orlando kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao

Orlando Nmsd.jpeg Orlando kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao

Tue, 23 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Orlando Pirates ya nchini Africa Kusini imefanikiwa kufuzu kucheza Ligi Ya Mabingwa kwa msimu ujao baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya nchini Afrika Kusini (PSL) nyuma ya vinara na mabingwa wa nchi hiyo, Mamelodi Sundown.

Hii ni baada ya Orlando kuifunga Amazulu FC anayoichezea Raly Bwalya aliyekuwa Simba kwa bao 4-0, mabao ya Orlando yakifungwa na Monyane dakika ya 5, Ratomo dakika ya 36, Saleng dakika ya 40 na Dlamini dakika ya 80.

Kutokana na hiyo, Afrika Kusini itawakilishwa na timu mbili katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa (CAFCL) msimu ujao ambao ni Mamelodi kama bingwa na Orlando kama mshindi wa pili.

Ikumbukwe kuwa katika, Mamelodi waliokuwa wakishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na kupewa nafasi kubwa na kuchukua ubingwa huo wameondolewa juzi katika hatua ya nusu fainali ya Wydad Casablanca ya Morocco.

Katika hatua nyingine, Klabu ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini iliyokuwa ikishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika imeondolewa na Yanga ya Tanzania katika hatua kama hiyo ya Nusu Fainali.

Aidha, Marumo maarufu kama Bahlabani ba Ntwa waliokuwa kwenye hali ngumu katika Ligi yao sasa rasmi wameshuka daraja baada ya kufungwa kufungwa bao 2 -0 na timu ya Swallows.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live