Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi: Manara akabidhiwa Kadi ya Uanachama Yanga

430de821885e92a48d567bacc9750874 Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara akikabidhiwa kadi yake ya Uanachama na Dkt Msolla

Thu, 28 Apr 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mseaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara amepatiwa rasmi kadi ya uanachama wa klabu hiyo.

Kadi hiyo iliyosajiliwa katika mfumo wa kielektroniki amekabidhiwa leo Aprili 28, 2022 na Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla.

“Hatimaye leo nimepata kadi yangu ya kwanza katika maisha yangu ya kuwa mwanachama kwenye klabu ya mpira nchini,” amesema Manara na kumshukuru Dk. Msolla na viongozi wengine, wadhamini na mashabiki.

Amesema yeye sasa ni mwanachama kamili wa Yanga, amepata amani ya moyo na jambo hilo limemuongezea nguvu kubwa katika kuitumikia klabu hiyo aliyojiunga nayo Agosti mwaka jana akitokea Simba ya Dar es Salaam.

Chanzo: www.habarileo.co.tz