Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi Mamadou Doumbia atua Yanga, atoa kauli nzito

Mamadou Doumbia Bnv Rasmi Mamadou Doumbia atua Yanga, atoa kauli nzito

Sun, 22 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki kisiki mpya wa Yanga na Timu ta Taifa ya Mali, Mamadou Doumbia amewaambia mashabiki wa klabu hiyo kuwa yeye sio mtu wa maneno sana bali ataacha vitendo vyake vizungumze uwanjani.

Doumbia amesema hayo mara baada ya kutua kwa miamba hao wa soka nchini wenye makazi yao mitaa ya Jangwani Kariakoo ambao wamemsajili akitokea katika timu ya Stade Malien ya nchini Mali kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.

Tayari beki huyu amesharipoti kambini maeneo ya Avic Town kwa ajili ya maandalizi kuelekea mchezo Jumatatu dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa katika uwanja wa Mkapa, kuanzia saa 1:00 jioni.

"Nimefurahi sana kufika hapa, Yanga ni klabu kubwa sana kule Mali, inafatiliwa na watu wengi hivyo kuja hapa ni jambo kubwa sana kwangu kama mchezaji.

"Mimi sio mtu wa maneno sana, kazi yangu ni uwanjani na mashabiki wategemee mazuri kutoka kwangu, nawapenda sana," alisema Doumbia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live