Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi: Kipre Jr ni mali ya USM Algier

Asx Kipreee Rasmi: Kipre Jr ni mali ya USM Algier

Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Mouloudia Club d'Alger, maarufu kama MC Alger ama MCA ya Algeria imekamilisha usajili wa aliyekuwa winga wa Azam Fc, Kipré Zunon Junior Kaa.

Azam imetangaza kumuuza Kipre Junior kwenda kwa Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Algeria wamempa Kipre mkataba wa miaka minne utakaomuweka klabuni hapo mpaka 2028.

Azam Fc itapokea kitita cha dola 300,000 (takribani milioni 797) kwa mauzo ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ivory Coast.

Msimu uliopita, nyota huyo alifunga magoli tisa (9) na kutoa assist tisa (9) kwenye mechi 28 alizocheza za NBC Premier League akitumia dakika 1630 akiwa na uzi wa Azam FC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live