Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi: Feisal atua Azam FC

Feisal Salum Winning Goal Rasmi: Feisal atua Azam FC

Sat, 24 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pesa inaongea! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia matajiri wa Chamazi, kudaiwa kumwaga mpunga mrefu na kufanikiwa kunasa Saini ya kiungo fundi Feisal Salum 'Fei Toto'ambaye alikuwa akiitumikia Yanga SC.

Taarifa zinaeleza kuwa, Feisal ambaye alikuwa na mkataba wa miaka minne na Yanga, amevunja mkataba rasmi jana kwa kuniandikia barua Yanga huku akiambatanisha na mzigo wa shilingi milioni 112 kama masharti ya mkataba.

Kipengele hicho cha mkataba alichokitumia Fei kinaeleza kuwa, endapo mchezaji atafikia kuvunja mkataba, atalazimika kulipa pesa ya kujiunga (signing fees) pamoja na mshahara wa miezi mitatu.

Hivyo Feisal ambaye inaaminika alikuwa analipwa mshahara wa shilingi milioni nne kwa mwezi, amelipa milioni 100 za singing fees pamoja na milioni 12 za mshahara wa miezi mitatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live