Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi Aziz KI athibitisha: Nitaendelea kusalia Yanga

AZIZ KI BADO YANGA Aziz KI.

Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz Ki raia wa Burkina Faso ametangaza rasmi kuwa ataendelea kusalia ndani ya viunga vya timu hiyo kwa msimu ujao baada ya kusaini mkataba mpya.

Kupitia kipande cha video kilichopostiwa na Yanga, Aziz amesema; "Hello Wananchi, am still here." Akimanisha "Habari Wananchi, nitaendelea kusalia hapa (Yanga)."

Aziz Ki amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga ambapo atapokea mshahara wa dola 13,000 sawa na shilingi milioni 35 za Kitanzania kwa mwezi.

Safu ya kiungo cha ushambuliaji ya Yanga msimu ujao itaundwa na Aziz Ki, Pacome Zouzoua, Clatous Chama, Maxi Nzengeli wakati mbele yao akimaliza 'Muuaji Anayetabasam' Prince Dube 'Mwana wa Mfalme'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live