Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rashford na rekodi tamu

Rashford Record Tamu.jpeg Rashford na rekodi tamu

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa timu ya taifa England, Marcus Rashford amekuwa mchezaji wa kwanza Manchester United kufunga mabao matatu kwenye fainali za Kombe la Dunia hatua ya makundi tangu mwaka 1966, Sir Bobby Charlton alipoweka rekodi hiyo.

Rashford alifunga mabao mawili dhidi ya Wales kwenye mechi ya mwisho hatua makundi England ikiibuka na ushindi wa mabo 3-0 na kufanikiwa kutinga raundi ya 16 bora ya fainali za Kombe la Dunia zinaoendelea huko Qatar.

Rashford alishangilia bao lake la kwanza alilofunga kwa mpira wa adhabu ndogo 'freekick' akimuenzi rafiki yake kipenzi Garfield Hayward aliyefariki hivi karibuni kwa ugonjwa wa kansa.

Nyota huyo alizungumzia bao hilo kwa huzuni baada ya mchezo huo akidai rafiki yale alifariki siku chache kabla ya mchezo wao dhidi ya England.

"Nimepoteza rafiki yangu wa karibu siku chache zilizopita, alikuwa anasumbuliwa na kansa kwa muda mrefu, nimefaurahi kwa sababu nimefunga bao kwa ajili yake, amenisapoti maisha yangu yote, amenionyesha upendo na nitamkumbuka siku zote," alisema Rashford.

Alipoulizwa na mwaandishi wa habari mabao hayo aliyofunga yanamaanisha kitu gani kwenye maisha yake, nyota huyo alijibu "Nadhani kubeba makombe ndio ndoto yangu kubwa, nafikiri kikosi kizima cha England mawazo yao ni ubingwa, tuna aina nyingi ya wachezaji wenye ubora hali ya juu, naamini tutaendeleza ubora wetu wa kufunga mabao na kushinda mechi, kikosi chetu kizuri na tuna uwezo kufukuzia ubingwa wa Kombe la Dunia,"

Mbali na rekodi hiyo Rashford yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa kiatu cha dhahabu Qatar baada ya kufunga mabao matatu akiwa sambamba na nyota wengine Kylian Mbappe (Ufaransa), Enner Valencia (Ecuador), na Cody Gokpo (Uholanzi).

Aidha kwa upande wa Valencia safari yake kwenye kinyang'anyiro hicho imefikia tamati kwani Ecuador imeondolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Senegal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live