Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rashford hatarini kutupwa benchi Man United

Rashford Vs Ten Hag Marcus Rashford

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Marcus Rashford yupo kwenye hatari ya kupigwa chini kwenye kikosi cha Manchester United kutokana na kucheza soka kwa kiwango cha hovyo msimu huu.

Staa huyo wa Man United msimu uliopita alifunga mabao 30. Lakini, mambo yamegoma msimu huu, ambapo hadi sasa amefunga bao moja tu, huku chama lake likikumbana na vipigo vitano katika mechi saba za karibuni.

Rashford alitolewa mapema katika mechi mbili zilizopita na huenda akapoteza nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza mbele ya Alejandro Garnacho au Anthony Martial wakati chama hilo litakapomenyana na Brentford kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uwanjani Old Trafford leo Jumamosi.

Kocha wa Man United, Erik ten Hag alisema: “Kuna timu halafu kuna yeye — halafu kuna wote. Ni sawa tu si kila nyakati unaweza kuwa kwenye viwango vya juu. Kila mtu anafahamu ubora wake. Tumemshuhudia akiwa bora kwenye nafasi yake. Haya ni mapito tu.”

Man United wanaamini straika Rasmus Hojlund atawasaidia kushinda mechi zao. Lakini, jambo kubwa linalowakabili ni safu yao ya ulinzi, ambapo mabeki wa kati watatu wa eneo hilo kwa sasa ni majeruhi.

Chanzo: Mwanaspoti