Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rashford hana presha kabisa

Marcus Rashford Rashford hana presha kabisa

Fri, 16 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Manchester united, Marcus Rashford, 25,  hana haraka ya kuitwa katika kikosi cha England kwani bado hayupo fiti kutokana na maumivu ya misuli yanaomsumbua.

Kocha wa England, Gareth Southgate  hakumjumuisha kikosini Rashford pamoja na Jadon Sancho anayecheza naye klabu moja.

Aidha kabla ya kuachwa kikosi cha England madaktari wa timu walikuwa wakimfuatilia hali yake, hata hivyo staa huyo amesisitiza hana haraka ya kuitwa kikosini kwani nafasi yake imechukuliwa na  Ivan Toney.

“Namtakia kila la kheri Ivan Toney, amepata nafasi ndani ya kikosi cha England, nasikitika sitashiriki mechi za Kimataifa kutokana na majeraha, kwasasa sipo tayari kwasababu bado sipo sawa,” alisema Rashford.

Rashford alipata maumivu ya misuli tangu mechi ya Ligi Kuu England, Manchester United ilipomenyana na Arsenal. Nyota huyo alifunga mabao mawili kwenye mchezo huu wakitoka na ushindi wa mabao 3-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live