Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rashford awatingishia Kiberiti Man United

Marcus Rashford 55 Marcus Rashford

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Straika wa Manchester United, Marcus Rashford anataka uhakika wa namba wa kudumu kikosini kabla ya kufanya maamuzi kuhusu hatima yake kwa mujibu wa ripoti.

Taarifa hiyo imeripotiwa na ripota maarufu wa masuala ya usajili Fabrizio Romano baada ya kupenyezewa na watu wa karibu wa nyota huyo.

Rashford mkataba wake utamalizika itakapofika mwaka 2023 yenye kipengele cha kuongoza mwingine lakini hatasaini hadi atakapopewa uhakika wa namba.

Nguli huyo wa masuala ya usajili ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa Rashford ameonyesha nidhamu ya hali juu kwani ni mchezaji ambaye amekulia katika kituo cha kukuzia vipaji Man United, hata hivyo kiwango chake bado hakijaridhisha tangu aliporejea baada ya kupona licha ya kufunga mabao manne Ligi Kuu England.

Ikumbukwe Rashford alikuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa bega.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz