Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rashford awapiga kibega PSG chap

Marcus Rashford England.jpeg Marcus Rashford.

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa, Marcus Rashford ameripotiwa atatupilia mbali ofa ya kwenda kujiunga na Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu huu ili aendelee kubaki zake Manchester United.

PSG iliaminika kwamba ingemshawishi Mwingereza huyo na kumsainisha ili akachukue mikoba ya Kylian Mbappe, huku ililenga kuwalipa Man United ada ya uhamisho ya Pauni 75 milioni.

Hata hivyo, wiki iliyopita, kocha wa Man United, Erik ten Hag alisema hakuna namna yoyote timu hiyo itafanya uamuzi wa kumuuza Rashford dirisha lijalo la usajili.

Na sasa, ripoti mpya zinafichua kwamba, hata Rashford, 26, mwenyewe hana mpango wa kuondoka Old Trafford dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi, hivyo atakataa ofa ya PSG ili aendelee na maisha yake jijini Manchester.

Man United inamtazama Rashford kama mchezaji wao muhimu kwenye mipango ya baadaye ikiwa chini ya bilionea Sir Jim Ratcliffe. Staa huyo alifunga bao lake la nane msimu huu, wakati Man United iliposhinda 4-3 dhidi ya Liverpool kwenye robo fainali ya Kombe la FA, Jumapili.

Rashford alifunga kufanya ubao wa matokeo usomeke 3-3 kwenye dakika ya 112 huko Old Trafford, kabla ya Amad Diallo kufunga bao la ushindi kwenye dakika ya 120 na Man United kushinda mchezo huo.

“Sikiliza hizo kelele, unaweza kuona ukubwa wa mechi hii na matukio kama haya. Sina msimu mzuri kama ninaotaka, lakini vitu kama hivyo vya hapa Old Trafford ni vizuri zaidi,” alisema Rashford.

Man United itakipiga na Coventry City kwenye nusu fainali ya Kombe la FA mwezi ujao, wakati vita ya kuhakikisha wanakuwa kwenye Top Four ili kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao itaendelea kwa mechi ya ugenini huko Brentford baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live