Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rashford ataja atakapocheza msimu ujao

Manchester United Vs West Ham Marcus Rashford Sends Red Devils 1024x576 Rashford ataja atakapocheza msimu ujao

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford ameripotiwa kuweka wazi mipango yake baada ya kuhusishwa kuwa anataka kuondoka timu hiyo.

Rashford ambaye hakufanya vizuri msimu uliopita akicheza mechi 43 za mashindano yote na kufunga mabao manane tu huku akiandamwa na kesi nyingi za utovu wa nidhamu nje ya uwanja, alikuwa akihusishwa kuondoka katika dirisha hili ili kujiunga na PSG ili akawe mbadala wa Kylian Mbappe.

Hata hivyo, Rashford anadaiwa kutaka kusalia Old Trafford kwa msimu ujao na amezungumza na kocha wa timu hiyo Erik ten Hag, akimwambia kwamba atabadilika na kuwa bora zaidi.

Kwa mujibu wa The Sun, Chanzo cha karibu na staa huyu kimesema, Ten Hag amemwambia Rashford kwamba bado yupo katika mipango yake.

“Anajua hajafanya vizuri sana lakini amekuwa akiwaambia marafiki zake kwamba atarejea kwa nguvu msimu ujao. Hataki kwenda popote na anataka kurejea katika ubora wake,” kilisema chanzo hicho.

Kiwango kibovu cha Rashford msimu uliopita pia kilimfanya aachwe nje ya kikosi cha England kinachoshiriki michuano ya Euro huko Ujerumani.

Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Rashford kuachwa katika kikosi cha England tangu apandishwe kwenye kikosi cha kwanza cha Man United, mara ya kwanza kuonekana katika michuano hii ilikuwa ni mwaka 2016 chini ya kocha Roy Hodgson.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa kuachwa kwenye kikosi cha Southgate kulimshangaza nyota huyo ambaye alidhani ataitwa.

“Marcus alijua nafasi yake ndani ya kikosi cha Gareth cha Euro ilikuwa hatarini kwani amekuwa na wakati mgumu msimu huu, lakini alishtushwa sana kutokuwepo hata katika kikosi cha awali.”

Chanzo: Mwanaspoti