Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rashford amekumbwa na nini?

Marcus Rashford Luke Shaw And Bruno Fernandes In Man Utd Training Rashford amekumbwa na nini?

Wed, 31 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Maofisa wa Manchester United wameanza kuwa na wasiwasi juu ya Marcus Rashford kutokana na kuzidiwa na maisha ya starehe kitu alichoanza kukifanya mwaka 2021 na kuhatarisha kipaji chake, imeelezwa.

Hofu kubwa imeibuka baada ya staa huyo kukesha kwenye pombe kwa siku mbili na kufanya sherehe mbalimbali nyumbani kwake akikusanya marafiki

Wayne Rooney, ambaye aliwahi kukumbwa na matatizo kama hayo wakati akiwa mchezaji, ameamua kumtafuta Rashford ili kuzungumza naye, ikiwa ni mpango wa kulinda kipaji cha mshambuliaji huyo.

Kinachoelezwa ni kwamba hata magwiji wengine wa Man United, David Beckham na Rio Ferdinand wamejaribu kumtafuta Rashford na kuwasiliana naye kutambua tatizo ni nini.

Magwiji hao wa England wameamua kumtafuta Rashford baada ya mabosi wa Man United kupata hofu kubwa kutokana na tabia za Rashford kwa kipindi cha karibuni, kwamba amezidisha starehe.

Kinachoripotiwa ni kwamba Rashford alilewa kwa saa 12 huko Belfast wiki iliyopita, kisha akapiga simu kudai kwamba anaumwa ili asiende mazoezini Ijumaa iliyopita.

Aliwekwa kando kwenye mchezo wa Jumapili iliyopita wa ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Newport kwenye Kombe la FA na atatozwa fainali ya mshahara wa wiki mbili, ambapo kwa wiki analipwa Pauni 325,000.

Alionyesha wasiwasi mkubwa baada ya kikao chake na kocha Erik ten Hag na mkurugenzi wa soka wa klabu hiyo ya Old Trafford, John Murtough, Jumatatu iliyopita.

Baada ya hapo, taarifa ya klabu ilisema kwamba kesi hiyo imemalizwa na kwamba anaweza kupewa nafasi ya kucheza kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Wolves utakaofanyika usiku wa leo, Alhamisi.

Kingine kilichowapa wasiwasi mabosi wa Man United ni baada ya mshambuliaji huyo kugombana na shabiki aliyekosoa kiwango chake kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid.

Alidaiwa kumfuata shabiki huyo na kumtolea lucha chafu kabla ya baadaye kukana kutenda tukio hilo.

Rooney, ambaye ni kama Rashford aliibuka kwenye soka na kutamba akiwa na umri mdogo sana, amejitole kumsaidia mshambuliaji huyo ili awe sawa na kutoka kwenye majanga hayo yanayoweza kumpoteza.

Chanzo kilibainisha: “Klabu imepata wasiwasi kutokana na mambo yanayoendelea. Na watu wake wa karibu na Marcus wanaamini kuna namna ya kufumbua jambo hilo na kama watamtumia Wayne akutane na kuzungumza na Marcus ana kwa ana. Wayne amelibali kutoa msaada huo. Marcus siku zote amekuwa akimtazama Wayne kama dira yake na shujaa wake, hivyo atazingatia kila kitu atakachoambiwa na gwiji huyo.” Rooney, ambaye kwa sasa amestaafu soka na alikuwa kocha wa Derby County, alimpigia simu Rashford. Kwa kuanza alimpa maneno ya kumpa moyo na kumwambia kwamba yeye yupo kama anahitaji ushauri zaidi wa kuonana. Rashford mwenyewe aliwahi kusema namna Rooney amekuwa akimpa sapoti kubwa kwenye maisha yake.

Rashford amedaiwa kucheza michezo ya kamari kwenye kumbi za starehe za usiku na kupiga sana kilaji.

Chanzo: Mwanaspoti