Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rashford alivyonusurika kifo kwa ajali

Rashford Alivyonusurika Kifo Kwa Ajali Rashford alivyonusurika kifo kwa ajali

Mon, 25 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambulizi wa Manchester United, Marcus Rashford alihusika katika ajali ya gari baada ya kuisaidia The Red Devils kupata 1-2 dhidi ya Burnley kwenye Uwanja wa Turf Moor siku ya Jumamosi jioni.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alikumbwa na ajali hiyo ambayo alinusurika na kutoka akiwa mzima alipokuwa akitoka kwenye uwanja wa mazoezi wa United wa Carrington, muda mfupi baada ya kikosi hicho kurejea kwenye kambi yao ya Mafunzo ya Carrington.

Nyota huyo alikuwa akiendesha gari lake moja kati ya matatu yake aina ya Rolls Royces, gari aina ya Black Badge Wraith ya Pauni 700,000 (zaidi ya Tsh. Bilioni 2.1).

Mwenzake Bruno Fernandes alionekana akiacha gari lake kisha kwenda kumsaidia Rashford, ambaye alionekana kuwa na hofu baada ya kugonga nguzo na gari lake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live