Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Marcus Rashford ameonekana kucharuka baada ya taarifa mbalimbali za uzushi kuenea kwenye mitandao ya kijamii juu ya mshahara wake na mkataba mpya.
Taarifa zimekua zikienea kumhusu mchezaji huyo huyo juu ya mkataba wake na klabu ya Manchester United, Huku zikieleza Rashford anahitaji mshahara mkubwa ndani ya klabu hiyo kipindi hichi ambacho mkataba wake unaelekea mwishoni mapema mwezi Juni mwaka huu.
Mshambuliaji huyo amefunguka kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram na kusema taarifa zinazosambaa kumhusu yeye na mshauri wake kuhusu kuhitaji maslahi zaidi ndani ya klabu ya Man United sio za kweli na mpango wake kwasasa upo kwenye kuisaidia klabu hiyo kushinda mataji zaidi ndani ya msimu huu.
Mshambuliaji huyo mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na taarifa zinaeleza yupo kwenye mazunguzmo na klabu yake ya Manchester United, Hivo taarifa hizo zimekua kwenye mzunguko mkubwa kwasasa na upotoshaji mwingine ukiendelea na kupelekea Marcus Rashford kukemea taarifa zinazosambaa mitandaoni.
Marcus Rashford amekua kwenye kiwango bora zaidi msimu huu na kuifanya klabu hiyo kua hatari kwenye eneo la ushambuliaji kutokana na mabao yake ambayo amekua akifunga ndani ya klabu hiyo, Hivo Manchester United wanataka kuhakikisha wanafanya kila kitu kumbakisha mchezaji huyo.