Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rashford: Nafurahi kufunga kwa ajili yake

Rsh Ford Goal Marcus Rashford alifunga mabao mawili mchezo dhidi ya Wales

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marcus Rashford amefichua sababu ya kihisia ya kushangilia bao lake la kwanza katika ushindi wa 3-0 wa England dhidi ya Wales.

Ulikuwa usiku wa kukumbukwa kwa mshambuliaji huyo wa Manchester United ambaye alifunga mabao mawili na kuhakikisha England inakamata nafasi ya kwanza katika Kundi B na kutinga hatua ya 16 bora.

Baada ya kufunga bao lake la kwanza, Rashford alipiga magoti na kunyooshea kidole anga katika kushangilia bao hilo kwa ajili ya rafiki yake Garfield Hayward, ambaye alifariki siku mbili kabla ya mchezo huo baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Wakati wa mahojiano yake baada ya mechi, alisema:

“Kwa bahati mbaya nilipoteza rafiki yangu mmoja siku chache zilizopita.

“Alikuwa na vita kwa muda mrefu na saratani, kwa hivyo ninafurahi nilifanikiwa kumfungia bao.

“Daima amekuwa mfuasi wangu mkubwa. Alikuwa tu mtu mkuu na nina furaha alikuja katika maisha yangu, kweli.” Alisema Rashford.

Rashford aliingizwa kwenye kikosi cha kwanza mara ya kwanza nchini Qatar na amempa Gareth Southgate maumivu ya kichwa wakati wa mechi yao ya hatua ya 16 bora dhidi ya Senegal siku ya Jumapili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live