Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raphinha kuwekwa sokoni Januari 2024

Raphinha.jpeg Raphinha kuwekwa sokoni Januari 2024

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabosi wa FC Barcelona bado wanahitaji kumuuza winga wao Raphinha mwenye umri wa miaka 26, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kushindwa kumuuza katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Winga huyo wa kimataifa wa Brazil amewekwa sokoni kwa sababu ya hali mbaya ya kiuchumi inayopitia klabu hiyo na kitendo cha staa huyu kupata majeraha ya mara kwa mara yanayosababisha awe nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Benchi la ufundi la FC Barcelona linataka kuchukua staa mwingine ambaye atatumika muda mwingi kuliko kumpa mshahara mkubwa Raphinha ambaye muda mwingi huwa nje.

Barca imepanga kumuuza winga huyu lakini kwa kiasi kisichopungua Euro 70 milioni na tayari baadhi ya timu kutoka England ikiwa pamoja na Chelsea na Arsenal zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili Raphinha ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 11 za michuano yote na kufunga mabao mawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live