Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raphael Varane atundika daruga Ufaransa

Raphael Varane Raphael Varane

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Klabu ya Manchester United, Raphaël Xavier Varane ametangaza Rasmi kustaafu kuitumikia Timu ya Taifa ya Ufaransa, akiwana umri wa miaka 29.

Varane ametangaza maamuzi hayo leo Alhamis (Februari 02), huku akikumbukwa kwa kuwa sehemu ya Kikosi cha Ufaransa kilichotwaa Ubingwa wa Dunia mwaka 2018 nchini Urusi, na kuisaidia nchi hiyo kufuzu Fainali za 2022 zilizonguruma nchini Qatar.

Varane ameweka rekodi yake binafsi kwa kucheza michezo 93 akiwa na Timu ya Taifa ya Ufaransa, ambayo kwa mara ya kwanza aliitumikia mwaka 2013, akipandishwa kutoka timu za Vijana.

Beki huyo ambaye alihamia Manchester United akitokea kwa Mabingwa wa Soka nchini Hispania Real Madrid, amefuata nyayo za Mlinda Lango wa Tottenham Hugo Lloris, ambaye alitangaza kustaafu kuitumikia Timu ya Taifa ya Ufaransa siku chache baada ya kutoka Qatar.

Akitumia Ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter Varane ameandika: “Umefika wakati kwa kizazi kipya kuchukua nafasi kwenye Timu ya Taifa ya Ufaransa”

“Naamini vijana wapo na wameandaliwa kwa ajili ya kuchukua nafasi kwenye kikosi cha Ufaransa, watapambana kwa ajili ya taifa letu na watastahili nafasi hiyo.”

Kuhusu Historia yake ya kutamani kuitumikia Ufaransa Varane ameandika: “Nakumbuka nikiwa na umri mdogo, mwaka 1998 Ufaransa tulikuwa mabingwa wa Dunia, nilitamani siku moja kuwa sehemu ya timu ya taifa, nashukuru ndoto zangu zilikuwa kweli.”

“Nilifanikiwa kwa miaka 20 iliyofuata kwa kuanza kuzitumikia timu za Taifa za Vijana, niliamini siku moja ningecheza Timu ya Taifa ya wakubwa, na kweli ilikuwa hivyo, hadi nikafikia ndoto uya kutwaa Ubingwa wa Dunia mwaka 2018!”

“Jambo la Msingi hapa ni kuisaidia timu yangu ya Taifa na kufikia ndoto zangu, niliamini hakuna linaloshindikana baada ya kufanikisha malengo yangu.”

“Daima sitasahau safari yangu. Bado ninakumbukwa siku ile ya Julai 15, 2018. Ilikua siku kubwa sana kwangu na kwa timu nzima ya Ufaransa, kwa sababu tulikuwa mabingwa wa Dunia, hii sitaisahau katika maisha yangu.”

“Kwa ushindi huo ninaamini tulishinda watu wote wa Ufaransa ambao kwa muda wote walikuwa nyuma yetu, kwa kutuombea mema, chini ya kocha wetu Didier Deschamps.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live