Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rangnick athibitisha Ronaldo Kuwakabili Atletico Madrid

Rangnick Kocha wa klabu ya Manchester United Ralf Rangnick

Tue, 15 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Manchester United Ralf Rangnick anaimani kuwa nyota wake Cristiano Ronaldo yupo tayari kuikabili klabu ya Atletico Madrid kwenye mashindano ya klabu bingwa ulaya kwenye dimba la Old Trafford.

Kwenye mchezo wa kwanza klabu ya Man Utd walifanikiwa kutoa sare nchini Hispania ya 1-1 dhidi ya Atletico Madrid ambapo goli la United lilifungwa na Anthony Elanga kwenye dakika za majeruhi na sasa wanacheza karata ya mwisho na mshindi wa mchezo huo atafanikiwa kwenda robo fainali ya michuano hiyo.

“Sina wasiwasi kwamba Ronaldo kuweza kuwa sawa kwenye mchezo dhidi ya Atletico Madrid,” alisema Rangnick.

“Mpaka sasa ameweza kujitunza yeye mwenyewe na kutunza mwili wake na anajua ni nini anachofanya, sina shaka kuhusu hilo. Ikiwa ataweza kufunga goli tatu nyingine, tutaona, namaanisha sio rahisi kufunga goli tatu dhidi ya timu zote.

“Nahisi uwezo wake ulikuwa mzuri, kama sio mzuri tutaona kesho tutakachokipata kutoka kwake kesho usiku. Lakini sio tu kuhusu Ronaldo, bali ni kuhusu timu nzima.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live