Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rangnick achukizwa na sare dhidi ya Newcastle United

Rangnick Fury Ralf Rangnick

Tue, 28 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ocha wa Manchester United Ralf Rangnick amekiri kuchukizwa na sare ya bao 1-1 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa dimba la Newcastle.

Kocha Rangnick amekiri hayo baada ya mchezo kumalizika ambapo amesema “sijafurahishwa na kiwango cha uchezaji hata baada ya kupata goli bado hatukuudhibiti mchezo vilivyo”, alisema.

Katika mechi hiyo, Manchester United walilazimika kusubili mpaka dakika za lala salama za kipindi cha pili kusawazisha goli kupitia kwa mshambuliaji Edinson Cavani ambaye aliingia kutokea bechi, Newcastle walitangulia kupata goli kupitia kwa Allan Saint-Maximin.

Bao la Cavani linampa nafasi Rangnick alama moja ambayo inamfanya kama kocha wa muda kutopoteza mechi ya kwanza hata hivyo pointi hiyo haimsaidii kwani kushindania nafasi ya nne bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live