Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rangnick aanza visingizio Man United

Ralf Rangnick Man Utd F365 9 Meneja wa Man United, Ralf Rangnick

Thu, 30 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa muda wa Manchester United Ralf Rangnick amesema janga la virusi vya Corona limechangia awe anashindwa kupiga hatua katika kuboresha kiwango cha timu hiyo kulinganisha na utawala uliopita.

Kocha huyo raia wa Ujerumani, hajafungwa mechi yoyote katika nne tangu alipombadili Ole Gunnar Solskjaer mwishoni mwa mwezi Novemba.

Licha ya kutofungwa kikosi hicho kimekuwa kama na ugonjwa wa msimu, akizungumzia hali hiyo amelitaja janga la Covid-19 kuwa chanzo moja wapo cha kurudisha nyuma ubora wa timu yake.

“Bila shaka hapana,” alisema Rangnick alipoulizwa kama amefikia malengo yake.

“Ili kupata ubora wa timu lazima ufanye mazoezi, sisi (Man United) tumekuwa hatufanyi”.

Katika kudhibitisha hilo, kocha huyo aliongea wazi kuwa hakufurahishwa na kiwango cha timu yake dhidi ya Newcastle United katika sare ya goli 1-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live