Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rangnick aanza na ushindi Old Trafford

Ralf Rangnick Gestures From The Touchline During His First Game In The Man Utd Dugout Ralf Rangnick aanza na ushindi United

Sun, 5 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tangu athibitishwe kuwa kocha mkuu wa Manchester United Ralf Rangnick amechukua jukumu la kuisimamia United katika mchezo wa EPL katika dimba la Old Trafford siku ya Jumapili dhidi ya Crystal Palace na goli pekee la Fred lilifanya mwanzo mzuri wa kocha huyo.

Fred alionyesha kiwango bora katika kipindi cha pili na dakika ya 77 aliweza kuwainua mashabiki wa United kwenye viti vyao, kwa kufunga bao safi kwa mguu wa kulia kutoka nje kidogo ya eneo la hatari.

Manchester United sasa wamesogea mpaka nafasi ya sita wakiwa na jumla ya alama 24 katika michezo 15 nyuma ya Tottenham ambao pia siku hiyohiyo waliibuka na ushindi safi wa 3-0 dhidi ya timu ya Norwich wanaoshika mkia katika jedwali la EPL.

Kituo kinachofuata kwa Red Devils ni Carrow Road wakiwafuata Norwich Jumamosi inayokuja Disemba 11 hivyo tutarajie muendelezo wa ushindi kwa upande wa Man United.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live