Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rangnick aanza na ushindi Austria

Ralf Rangnick 123 Kocha wa Timu ya Taifa ya Austria

Sat, 4 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mpya wa timu ya taifa ya Austria Ralf Rangnick ameanza kwa ushindi mnono na timu ya taifa ya Austria kwa kuicharaza 3-0 Croatia katika michuano ya UEFA Nations League ya mwaka huu.

Baada ya kumaliza muda wake na klabu ya Manchester United Rangnick ilisemekana ataendelea kushirikiana na United akiwa kama mshauri wa klabu lakini baadaye alipiga chini majukumu hayo na kuangazia zaidi majukumu ya ukufunzi na timu ya taifa ya Austria.

Rangnick amekuwa kocha wa kwanza wa Austria kuiongoza kupata ushindi na clean sheet tangu mwaka 2002 ambapo Hans Krankl alikuwa kocha timu hiyo.

Akizungumza baada ya mchezo kumalizika, Rangnick alisema alifurahishwa na jinsi timu yake ilivyokabiliana na Croatia na kuibuka ushindi.

“Tulikuwa na matatizo katika dakika 25 za kwanza, lakini kupata bao la kuongoza kabla ya mapumziko kulitusaidia vyema,” alisema.

“Kipindi cha pili tulicheza vizuri sana na tukafunga mabao mawili mazuri – tungeweza kufunga zaidi.

“Nimeridhika sana.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live