Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ramsdale kukabiliwa na upinzani Arsenal

Image 65 1140x640.png Ramsdale kukabiliwa na upinzani Arsenal

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: Dar24

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anapanga kumpa nafasi David Raya badala ya kipa namba moja Aaron Ramsdale katika mechi ijayo ya Ligi Kuu England.

Arteta alifanya usajili wa kushtua wa kipa huyo licha ya kuwa na Ramsdale ambaye amekuwa maarufu Arsenal kwa sasa kutokana na mchango wake.

Lakini, chanzo kimeripoti kuwa ni suala la muda kabla ya Arteta hajafanya uamuzi wa kumpa nafasi Raya aliyejiunga akitokea Brentford kwa mkopo wa muda mrefu.

Arteta ni shabiki mkubwa wa Raya kutokana na uwezo wake na imeonekana kocha huyo atampa nafasi katika mechi zinazofuata.

Kipa huyo atakosa mechi ya Kombe la Carabao dhidi ya Brentford kutokana na sheria za Ligi Kuu kwa sababu hapaswi kucheza kwa mkopo dhidi ya timu aliyotokea.

Ramsdale alisaini mkataba Mei, mwaka huu na anatambua ushindani uliopo kati yake na Raya siku zijazo hivyo anachotakiwa ni kukaza buti.

Kutokana na usajili wa kipa huyo mpya, Arteta alipondwa, lakini alimlinda na kumtetea akisema hakuna tatizo: “Sioni tatizo kuhusu usajili huu. Kuwa na makipa wawili wazuri sio tatizo ipo wazi tunataka kuwa bora kila siku na mazingira yanatakiwa kubadilika,” alisema.

Chanzo: Dar24