Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ramsdale atoke vipi Arsenal

Arsenal Goalkeepers Aaron Ramsdale David Raya Ramsdale atoke vipi Arsenal

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndo hivyo mambo si mambo kwa kipa wa Aaron Ramsdale huko kwenye kikosi cha Arsenal na sasa kipa huyo anapiga hesabu za kutafuta makazi mapya ya kwenda kukipiga kunusuru soka lake.

Kipa huyo Mwingereza, 25 aliwekwa tena kando na Kocha Mikel Arteta katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo Arsenal iliichapa Sevilla 2-1 na sasa anafikiria itakuwa vipi wakati huu akiwa kwenye mapambano ya kuwa vizuri ili apate nafasi ya kucheza Euro 2024.

Kocha Arteta ameendelea kumwaamini David Raya, ambaye amemsajili kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Brentford, Agosti mwaka huu.

Ramsdale hajacheza mechi yoyote ya Ligi Kuu England au michuano ya Ulaya tangu mwanzoni mwa Septemba mwaka jana kwa sababu Kocha Arteta ameweka imani yake kwa kipa Raya, 28. Mechi pekee ambayo Ramsdale alicheza ni ile ya Kombe la Ligi dhidi ya Brentford kwa kuwa Raya hapaswi kucheza dhidi ya timu yake.

Chelsea; Miamba hiyo ya Stamford Bridge inafikiria kunasa saini ya Ramsdale kwenye dirisha la Januari na bosi wao, Todd Boehly wala hana shida kwenye kutumia pesa. Kipa namba moja wa Chelsea kwa sasa ni Robert Sanchez, lakini Mhispaniola huyo alikuwa chaguo la tatu Brighton kabla hajatua Stamford Bridge.

Bayern Munich; Kama Arsenal itagoma kumuuza Ramsdale kwenye Ligi Kuu England. Bayern Munich inahitaji kipa kwa sababu Manuel Neuer bado hajapona vyema mguu na haifahamiki kama atakaporudi atakuwa kwenye ubora wa kutosha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live