Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ramsdale: Inaniuma kupoteza nafasi Arsenal

Raya X Ramsdale Ramsdale: Inaniuma kupoteza nafasi Arsenal

Sat, 21 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Mlinga Lango Aaron Ramsdale amesema “nateseka na kuumia” baada ya kupoteza nafasi katika kikosi cha kwanza cha Arsenal kwa David Raya, lakini akasisitiza yeye na mwenzake wako kwenye mahusiano mazuri.

Ramsdale alikuwa chaguo la kwanza tangu ajiunge na timu hiyo mwaka 2021 na alicheza mechi zote 38 za Ligi Kuu England msimu uliopita, lakini aliwekwa benchi kwenye mechi nne za mwisho za ligi ya timu hiyo ya London Kaskazini huku Raya, ambaye aliwasili kwa mkopo kutoka Brentford Agosti mwaka huu akichukua nafasi yake.

“Nadhani kwa sababu ni mara ya kwanza kutokea na hali imekuwa ngumu,” alisema Ramsdale akiwaambia waandishi wa habari.

“Ikiwani mimi au David ambaye anacheza tunahitaji kuwa na uwezo wa kuzingatia tu na kucheza. Tunapaswa kukabiliana nayo na ndivyo tunafanya. Tunafanya kazi pamoja kitaaluma vizuri sana.

Ramsdale aliitwa kwenye kikosi cha Kocha, Gareth Southgate cha England kwa mechi ya kirafiki mwezi huu dhidi ya Australia na kufuzu euro 2024 dhidi ya Italia, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hakucheza katika mechi zote mbili.

“Kwangu mimi nahitaji kurejea katika timu yangu ili kuendelea kuchaguliwa kwa ajili ya England na kuendelea kuumiza kichwa kwa kocha kwa sababu kama sichezi, basi huo ni uamuzi rahisi kwake, aliongeza Rarnsdale. Ni wasiwasi, ni mara ya kwanza kujikuta katika hali hii.”

Arsenal, ambao wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu England watasafiri kumenyana na Chelsea baadae leo Jumamosi (Oktoba 21).

Chanzo: Dar24